-
-
by
Victor Abuso
Shirikisho la soka nchini Kenya FKF, limetangaza rasmi kuanza kusimamia usajili wa wachezaji wote wakaocheza katika ligi zote nchini humo na wale watakaokuwa wanakwenda kucheza soka nje ya nchi.
FKF inasema imeamua kuchukua jukumu hilo ili kusimamia kikamilifu kanuni za Shirikisho la soka duniani FIFA, na itaanza kutekelezwa kuanzia tarehe 2 mwezi Juni mwaka huu wakati wa usajili wa dirisha dogo.
Kanuni ya FIFA, inasema kuwa Shirikisho la soka katika nchi husika itasimamia usajili wa wachezaji watakaocheza soka nchini humo lakini pia kufuatilia maendeleo yao.
FKF inasema mabadiliko haya yatasaidia usawa na urahihishaji wa usajili wa wachezaji hao.
Hata hivyo, uongozi wa soka nchini humo unasema usajili ambao ulifanywa na kampuni inayosimamia ligi KPL, wataendelea kutambuliwa na FKF.
Pamoja na hilo, wadau wote wanaoandaa michuano mbalimbali ya soka wametakiwa kulifahamisha Shirikisho la soka FKF.



Africa Cup of Nations
Teams get tough opponents in AFCON 2025 Draws

Africa Cup of Nations
Tanzania,Uganda in tricky group with Nigeria and Tunisia

Africa Cup of Nations
Tough Afcon Group B as SouthAfrica paired with Egypt,Angola,Zimbabwe

Africa Cup of Nations
Teams get tough opponents in AFCON 2025 Draws

Africa Cup of Nations
Tanzania,Uganda in tricky group with Nigeria and Tunisia

Africa Cup of Nations
Tough Afcon Group B as SouthAfrica paired with Egypt,Angola,Zimbabwe
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...