Connect with us

Shirikisho la soka nchini Kenya FKF, limeiandikia barua Shirikisho la soka barani Afrika CAF, kulalamikia uonevu wa wa marefarii katika mchuano wa kufuzu kucheza fainali ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2019 nchini Cameroon dhidi ya Sierra Leone Jumamosi iliyopita.

Harambee Stars ikicheza ugenini jijini Freetown ilifungwa mabao 2-1 na wenyeji wao.

Rais wa FKF Nick Mwendwa ameiambia tovuti ya michezo kutoka nchini Kenya Soka25east.com, kuwa hawakuridhishwa na maamuzi yaliyotolewa na marefarii hao.

Mchuano huo ulioongozwa na marefarii kutoka nchini Nigeria, wakiongozwa na refarii wa kati Ferdinand Aniette pamoja na wasaidizi wake Tejiri, Abdulmajeed Olaide na Ekabatiem Ekabatiem.

Aidha, Kenya imekasirishwa na hatua ya beki wake Brian Mandela, kupewa kadi nyekundu katika mchuano huo baada ya refarii kudai kuwa alimchezea ndivyo sivyo mshambuliaji wa Sierre Leone Alhassan Kamara .

Rais wa FKF, ameeleza kuwa anaamini kuwa hata baada ya kuiandikia barua CAF, anafahamu kuwa hakuna maamuzi yoyote ambayo huenda yakachukuliwa dhidi ya marefarii hao au hata kubadilisha matokeo lakini anachotaka ni malalamishi yao kusalia katika kumbukumbu ya CAF.

More in