Shirikisho la soka nchini Gabon limemsimamisha kazi kocha wa timu ya taifa ya soka Jorge Costa .
Hatua hii inakuja miezi miwili kuelekea nchi hiyo kuwa wenyeji wa michuano ya kufuzu kucheza fainali ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka ujao.
Nafasi ya kocha huyo imechukuliwa sasa na Mkurugenzi wa kiufundi wa timu ya taifa, Jose Antonio Garrido.
Shirikisho la soka nchini humo halijatoa sababu yoyote ni kwanini imeamua kumsimamisha kazi kocha huyo mwenye umri huyo wa miaka 45 kutoka nchini Ureno.
Hatua hii inakuja baada ya kuteuliwa tena kuifunza Gabon kwa miezi sita baada ya mkataba wake kukamilika mwezi Juni.
Kocha huyu mpya ana wiki moja tu kuiandaa Gabon kumenyana na Mali katika mchuano wa kufuzu kucheza kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Gabon wamepangwa katika kundi la A na mabingwa mara nne wa bara Afrika Cameroon, Burkina Faso iliyomaliza ya pili mwaka 2013 na Guinea-Bissau.