Ghana ipo hatarini kupoteza nafasi ya kuwa mwenyeji wa michuano ya soka barani Afrika kwa upanda wa wanawake kutokana na sintofahamu iliyotokea baada ya kujiuzulu kwa rais wa Shirikisho la soka nchini humo Kwesi Nyantakyi kwa tuhma za ufisadi.
Duru zimeiambia www.soka25east.com kuwa Kenya imeonesha nia ya kuwa mwenyeji wa michuano hiyo mikubwa na Shirikisho la soka barani Afrika CAF, linaangalia uwezekano wa kuhamishia mashindano hayo jijini Nairobi.
Miezi minne kuelekea mashindano hayo ambayo yameratibiwa kuanza kati ya tarehe 17 mwezi Novemba hadi tarehe 1 mwezi Desemba, CAF haijafurahishwa na maandalizi yanayoendelea.
Kenya ilipoteza nafasi ya kuandaa mashindano ya CHAN, mapema mwaka huu na nafasi hiyo kuchukuliwa na Morocco kwa sababu ya maandalizi mabaya haya ukosefu wa viwanja.