Michuano ya mzunguko wa pili kufuzu hatua ya makundi kuwania taji la Shirikisho barani Afrika inachezwa siku ya Jumanne na Alhamisi katika mataifa mbalimbali.
Baada ya kuanza vema nyumbani, kwa kupata ushindi wa bao 1-0, dhidi ya CS La Mancha ya Congo Brazaville, AS Vita Club itakuwa ugenini kujaribu kupata ushindi wa pili.
USM Alger ya Algeria, iliyoanza vibaya ugenini dhidi ya Plateau Unted ya Nigeria kwa kufungwa mabao 2-1, itakuwa nyumbani kutafuta ushindi muhimu.
Ratiba nyingine Jumanne Aprili 16 2018:-
Belouizdad (Algeria) vs ASEC Mimosas (Cote Dvoire)
Al Masry (Misri) vs Mounana (Gabon)
Wawakilishi wa Kenya Gor Mahia, ambao wamekuwa wakikumbwa na changamotoya baadhi ya wachezaji wake kukosa visa ya kwenda Afrika Kusini kumenyana na SuperSport United, imekuwa ikifanya maandalizi ya lala salama.
Mkurugenzi Mtendaji wa klabu hiyo Omondi Aduda amethibitsiha kuwa kikosi cha Gor Mhaia kitaondoka jijini Nairobi Jumanne usiku bila ya wachezaji wao wa kutegemewa Jacques Tuyisenge, Ephraim Guikan na Francis Kahata ambao wamekosa visa kwa sababu zisizoeleweka.
Mechi ya kwanza wiki moja iliyopita mjini Machakos, Gor Mahia ilipata ushindi wa bao 1-0.
Ratiba siku ya Jumatano Aprili 17 2018:-
Welayta Dicha vs Young Africans
CARA Brazaville vs Saint George
Akwa United vs Al Hilal Omdurman
SuperSport United vs Gor Mahia
Costa do Sol vs Rayon Sport
Raja Casablanca vs Zanaco.