-
-
by
Victor Abuso
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ameahidi kuwatafutia ufadhili mabingwa wa ligi kuu ya soka nchini humo Gor Mahia baada ya kunyakua ubingwa nchini humo kwa mwaka wa tatu mfululizo.
Odinga akiwa katika chakula cha mchana na mabingwa hao siku ya Jumanne jijini Nairobi, amekabidhi klabu hiyo Kitita cha Shilingi za Kenya 500, 000.
Wachezaji wamegawana Shilingi 300,000 huku Benchi ya kiufundi ikikabidhiwa 100,000 na Mwenyekiti wa klabu hiyo Ambrose Rachier na wenzake wakigawana Shilingi 100,000.
“Tunajitahidi sana kuhakikisha kuwa Gor Mahia inapata mfadhili msimu ujao. Sitaki kutaja ni kampuni gani tunayozungumza nayo lakini fahamuni kuwa mambo mazuri yapo njiani,” alisema Odinga.
Odinga ambaye ametoa changamoto kwa mabingwa hao ambao wameibuka washindi mwaka huu bila kufungwa hata mchuano mmoja,kufanya vizuri katika mashindano ya klabu bingwa barani Afrika mwaka ujao.
Gor Mahia ilimaliza ligi Jumapili iliyopita kwa ushindi wa mabao 2 kwa 0 dhidi ya Muhoroni Youths katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi, na kukabidhiwa kombe.



Africa Cup of Nations
Teams get tough opponents in AFCON 2025 Draws

Africa Cup of Nations
Tanzania,Uganda in tricky group with Nigeria and Tunisia

Africa Cup of Nations
Tough Afcon Group B as SouthAfrica paired with Egypt,Angola,Zimbabwe

Africa Cup of Nations
Teams get tough opponents in AFCON 2025 Draws

Africa Cup of Nations
Tanzania,Uganda in tricky group with Nigeria and Tunisia

Africa Cup of Nations
Tough Afcon Group B as SouthAfrica paired with Egypt,Angola,Zimbabwe
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...