Connect with us

Gor Mahia yapokonywa alama 3

Gor Mahia yapokonywa alama 3

 

Kamati ya nidhamu ya kampuni inayosimamia ligi kuu ya soka nchini Kenya KPL, imeamuru mabingwa watetezi wa ligi hiyo Gor Mahia ,kupokonywa alama tatu baada ya mashabiki wake kuzua fujo wake wa mchuano wake na Tusker FC mwezi Aprili katika uwanja wa Taifa wa Nyayo jijini Nairobi.

Mbali na adhabu hiyo kwa Gor Mahia, kipa wake Boniface Olouch amefungiwa kutocheza mchuano mmoja baada ya kumvamia mshika kibendera, mechi ambayo Tusker FC walishinda bao 1 kwa 0.

Kamati hiyo imebaini kuwa, klabu ya Gor Mahia ilishindwa kuwadhibiti mashabiki wake walioingia uwanjani na kuanza kumkimbiza mwamuzi msaidizi na kusimamisha mechi hiyo kwa dakika 10 baada ya Tusker kupewa penalti.

Pamoja na hilo, Kamati hiyo imesema haijaridhishwa na namna Gor Mahia inavyowadhibiti wachezaji wake wakati wa michuano mbalimbali na hivyo kuzua hofu uwanjani.

Kwa adhabu hii, Gor Mahia ambayo ilipanda kileleni mwa ligi kuu siku ya Jumatano wiki hii  kwa alama 29 inashuka hadi katika nafasi ya pili kwa alama 26 nyuma ya Tusker FC ambayo ina alama 29.

 

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in