Connect with us

Gor Mahia yasaka historia Nigeria

Gor Mahia yasaka historia Nigeria

Na Victor Abuso,

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka nchini Kenya Gor Mahia, wanahitaji kulinda ushindi wa mabao 3-1 waliopata dhidi ya klabu ya Lobi kutoka nchini Nigeria wiki iliyopita, ili kuandika historia ya kufuzu katika hatua ya makundi kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika.

Mechi hiyo ya marudiano itachezwa siku ya Jumamosi, mjini Enugu na Gor Mahia wanahitaji sare na kuzuia kufungwa katika mechi hiyo ili kufuzu, chini ya kocha wake mpya Hassan Oktay.

Hata hivyo, mabingwa hao mara 17 wa soka nchini mwao watakosa hudumu muhimu za kiungo wa kati Ernest Wendo ambaye katika anatumia adhabu ya kadi mbili za njano.

Gor Mahia, iliyoshinda kombe la Mandela mwaka mwaka 1987, haijawahi kufika katika hatua ya makundi tangu kuanzishwa kwa mfumo mpya wa kufuzu katika hatua hiyo.

Mechi nyingine muhimu Jumamosi Desembe 22 (Klabu bingwa):

ZESCO United vs TP Mazembe

Vipers vs CS Constantine

Jumapili

Simba vs Nkana.

Taji la Shirikisho Jumamosi Desembe 22:-

FS San Pedro vs DC Motemba Pembe

Asante Kotoko vs Kariobangi Sharks

Mukura Victory Sports vs Al-Hilal Al-Ubayyid

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in