Connect with us

Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limeamua kuwa timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Kenya itashiriki katika fainali za bara Afrika, zitakazofanyika nchini Ghana mwezi ujao.

Hatua hii imekuja baada ya CAF, kuindoa Equatorial Guinea kwa sababu imebanika kuwa, ilitumia wachezaji sita ambao hawakustahili kuichezea wakati wa michuano ya kufuzu, mmoja akiwa mchezaji wa Cameroon, kinyume na utaratibu wa Shirikisho la soka barani Afrika.

Equatorial Guinea ilikuwa imefuzu katika fainali hiyo baada ya kuifunga Kenya mabao 3-2 katika mechi yake ya mwisho kuelekea nchini Ghana.

Itakuwa ni mara ya pili Kenya kushiriki katika mashindano haya, ilikuwa ni mwaka 2016 nchini Cameroon.

Kenya sasa inaugana na mataifa mengine kama Algeria, Cameroon, Nigeria, Mali, Afrika Kusini na Zambia katika fainali hizo zitakazofanyika kati ya tarehe 17 mwezi Novemba hadi na tarehe moja mwezi Desemba.

 

 

More in East Africa