Kocha wa timu ya taifa ya soka Kenya Harambee Stars Bobby Williamson, amewaita viungo wa kati Peter Nzuki wa Nakumatt FC na Kevin Amwayi wa Ulinzi Stars katika kikosi cha wachezaji 20 kujiandaa kwa mchuano wa mzunguko wa kwanza kufuzu katika kombe la duniani mwaka 2018 dhidi ya Mauritius.
Nahodha wa zamani Dennis Oliech, mfungaji bora wa ligi kuu Jesse Were, Lawrence Olum, Francis Kahata na Paul Were wameachwa katika kikosi hicho kitakachoanza mazoezi yake siku ya Ijumaa jijini Nairobi.
Hata hivyo, kocha huyo amewaita wachezaji waliocheza na Zambia katika mchuano wa kufuzu katika kombe la mataifa bingwa barani Afrika mapema mwezi huu huku mchezaji wa Southampton Victor Wanyama akisalia kuwa nahodha.
Duru zinasema kuwa Jesse Were na Dunson Kago waliachwa nje katika kikosi hicho kwa sabbau za kinidhamu.
Mshambuliaji wa Gor Mahia, Allan Wanga anayechezea klabu ya Azam ya Tanzania na Jacob Kelli amesalia katika kikosi hicho.
Kikosi kamili:
Makipa:- Arnold Origi (Lillestrom, NOR), Boniface Oluoch (Gor Mahia, KEN)
Mabeki:- David Owino (Zesco Utd, ZAM), David Ochieng’ (Hana klabu), Dennis Odhiambo (Thika Utd, KEN), Brian Mandela (Maritzburg Utd, Afrika Kusini), Edwin Wafula (AFC Leopards, KEN)
Viungo wa Kati:- Bernard Mang’oli (AFC Leopards, KEN), Peter Nzuki (Nakumatt, KEN), Kevin Amwayi (Ulinzi, KEN), Johanna Eric Omollo (Mathare Utd, KEN), Abdul Latif (Bandari FC, KEN), Teddy Akumu (Al Khartoum, SUD), JOhanna Ochieng Omollo (Royal Antwerp, UBELG), Victor Wanyama (Southampton, UINGEREZA), Ayub Timbe (SK Lierse, UBELGIJI)
Washambuliaji:- Michael Olunga (Gor Mahia, KEN), Allan Wanga (Azam FC, TZ), Jacob Kelli (Nkana Red Devils, ZAM)