Na Fredrick Nwaka,
Dar es Salaam. Klabu ya Simba imesema bado ina imani kubwa na benchi la ufundi la ufundi na haina mpango wa kulifumua.
Simba iliyotumia bilioni 1.3 za Tanzania kufanua usajili ilibanwa mbavu na Yanga kwa kutoka sare ya bao 1-1 hatua iliyozua hasira kwa mashabiki wanaoshinikiza klabu hiyo kumtia Kocha wake Joseph Omog.
Akizungunza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam Leo Ofisa Habari na Mawasiliano wa Simba Haji Manara alisema hakuna mpango wowote wa kumwondoa Omog.
“Hakuna mabadiliko yoyote kwa makocha wetu tunaendelea na Joseph Omog na Masoud Juma,”amesema Manara.
Wakati huohuo klabu hiyo imeelezea kusikitishwa na maamuzi yanayotolewa na baadhi ya waamuzi katika michezo ya Ligi Kuu.
“Mechi na Yanga tulinyimwa penati na mwamuzi akiwa anaona baada ya Yondani kuunawa mpira kwenye eneo la hatari, pia mechi na Mbao na Stand tulinyimwa penati za wazi,”amesema Manara anayesifika kwa kuongea sana.
Simba inajiadaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City utakaochezwa mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Uhuru.