Rais wa zamani wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF, Issa Hayatou na aliyekuwa Katibu Mkuu Hicham El Amrani wametozwa faini ya Dola Milioni 27.9 kila mmoja na Mahakama ya Uchumi nchini humo EEC.
Mahakama hiyo imesema kuwa wawili hao walivu ja sheria ya nchi hiyo kwa kutia saini mkataba wa Dola Bilioni Moja kati ya CAF na kampuni ya Ufaransa ya Lagardere mwaka 2015.
Sheria ya Misri, inasema kuwa, kupata mkataba huo, lazima uwe wazi kwa kila mmoja lakini haikuwa hivyo.
Hata hivyo, El Amrani na Hayatou wamesema kuwa, watakata rufaa kuhusu faini hyo.
Aidha, wanasema kuwa kesi hiyo imechochewa kisiasa.