Bakary Papa Gassama kutoka nchini Gambia, kwa mwaka wa pili mfululizo ameshinda tuzo ya refarii bora barani Afrika.
Gassama mwenye umri wa miaka 36 alikuwa refarii wa FIFA mwaka 2007 na mwaka 2012 alikuwa miongoni mwa marefarii walioshiriki katika michuano ya Olimpiki na hasa fainali kati ya Mexico na Brazil lakini kipindi hicho alikuwa afisa wanne katika mchuano huo.
Mwaka 2012 na 2013 alichezesha michuano ya mataifa bingwa barani Afrika pamoja na fainali za kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil.
Mwezi Machi mwaka 2013 Shirikisho la soka duniani FIFA, lilimteua Gassama kuwa miongoni mwa marefarii 50 waliokuwa wameteuliwa kuwa waamuzi wa michuano ya kombe la dunia.
Januari tarehe 15 mwaka 2014 miezi kadhaa kabla ya kombe la dunia, Gassam alichaguliwa kuwa miongoni mwa wamuuzi 25 waliopewa jukumu la kucheza kombe la dunia nchini Brazil.
Alichezesha mchuano wa makundi kati ya Uholanzi na Chile.
Mchuano wake wa mwisho kuchezesha ilikuwa ni fainali ya kombe la mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2015, tarehe 8 kati ya Ghana na Ivory Coast nchini Equitorial Guinea.
Orodha kamili
2015 Bakary Gassama-Gambia
2014 Bakary Gassama-Gambia
2013 Djamel Haimoundi-Algeria
2012 Djamel Haimoundi-Algeria
2011 Noumandiez Doue-Cote d’Ivoire.