Kombe la dunia ni mashindano ya Kimataifa ya mchezo wa soka baina ya wanaume wanaowakilisha mataifa yao.
Michuano hii imekuwa ikichezwa tangu mwaka 1930 nchini Uruguay, chini ya usimamizi wa Shirikisho la soka duniani FIFA.
Fainali ya mwaka 2018 nchini Urusi, itakayofanyika kati ya tarehe 14 mwezi Juni hadi 15 mwezi Julai, itakuwa ya 21 katika historia ya michuano hiyo.
Michuano hii, hufanyika kila baada ya miaka minne.
Orodha ya Mataifa ambayo yamewahi kuwa wenyeji wa fainali ya kombe la dunia:-
1930-Uruguay
1934-Italia
1938-Ufaransa
1950-Brazil
1954-Switzerland
1958-Sweden
1962-Chile
1966-Uingereza
1970-Mexico
1974-West Germany
1978-Argentina
1982-Uhispania
1986-Mexico
1990-Italia
1994-Marekani
1998-Ufaransa
2002-Korea Kusini na Japan
2006-Ujerumai
2010-Afrika Kusini
2014-Brazil
2018-Urusi
Historia ya washindi wa kombe la dunia:-
Brazil-Mara 5 (1958,1962,1970, 1994 na 2002)
Ujerumani-Mara 4 (1954,1974,1990,2014)
Italia-Mara 4 (1934,1938,1982,2006)
Argentina-Mara 2 (1978,1986)
Uruguay-Mara 2 (1930,1950)
Ufaransa-Mara 1 (1998)
Uingereza-Mara 1 (1966)
Uhispania-Mara 1 (2010)