-
by
Victor Abuso
Mashabiki wa klabu ya AS Vita Club wamekasirishwa na hatua ya klabu yao kuondolewa katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika katika dakika za lala salama.
Vita club yenye makao yake jijini Kinshasa, iliondolewa siku ya Jumanne kwa kosa la kumchezesha Idrissa Traore aliyekuwa amefungiwa na Shirikisho la soka barani Afrika CAF kucheza mechi nne.
Malalamishi hayo yaliwasilishwa kwa CAF na klabu ya Stade Malien ambayo mchezaji huyo alikuwa anaichezea kabla ya kwenda AS Vita Club.
Traore aliitumikia adhabu ya mchezo mmoja wakati akiichezea Stade Malien, lakini akaichezea klabu ya Mamelodi Sundowns na kuisaidia klabu yake kushinda.
Mchezaji huyo pia aliwahi kuichezea klabu ya Zanzibar Mafunzo FC katika hatua ya awali ya michuano hii.
Aidha, ni habari mbaya kwa mchezaji wa kimataifa wa Rwanda Ernest Sugira ambaye hivi karibuni alisajiliwa na klabu hiyo na kuwa na matumaini ya kuonesha ushapavu wake katika michuano hii mikubwa barani Afrika.
Mashabiki wa klabu hii wanahoji inakuwaje kuwa hawakufahamu kuwa mchezaji huyo alikuwa amefungiwa lakini pia inakuwaje, mchezaji mwenyewe alikubali kucheza akiwa anafahamu kuwa amefungiwa kucheza mechi nne.
CAF Confederation Cup
Simba snatch late winner against CS Sfaxien as Enyimba beaten
CAF Champions League
Sundown CL campaign has a pulse after beating Raja
CAF Champions League
TP Mazembe win CAF Women’s Champions league trophy
CAF Champions League
Mamelodi Sundowns Off to a Lukewarm Start in 2024/25 CAF Champions League
CAF Champions League
AL Ahly start CAF CL campaign with win over Stade d’Abidjan
CAF Confederation Cup
Simba make good start beating Bravos do Maquis
CAF Confederation Cup
Enyimba fall to Al Masry in Alexandria
CAF Confederation Cup
Zamalek got their Group D campaign off to a comfortable star
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...