Rais wa Shirikisho la Soka Duniani Gian Infantino amewasili Tanzania alfajiri ya leo na kulakiwa na viongozi mbalimbali wa serikali na Shirikisho la Soka Tanzania TFF. Ameambatana na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika CAF, Ahmad Ahmad.
Katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, Infantino amelakiwa na Waziri wa Haabari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe, Rais wa TFF, Wallace Karia na mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa Leodgar Tenga.
Katika mkutano huo Fifa inatarajia kujadili mipango mbalimbali ya maendeleo kwa mataifa ya Afrika.
Akizungumza baada ya kumpokea kiongozi huyo Waziri Mwakyembe amesema Tanzania iko tayari kutoa ushirikiano kwa mikakati mbalimbali ya Fifa yenye lengo la kuinua soka la Afrika.
“Tunawaunga mkono na Tanzania iko tayari kushirikiana na Fifa, tunawatakia mkutano mwema na tunawahakikishia amani na usalama katika muda wote watakaokuwa hapa,”alisema Mwakyembe.
Mkutano huu wa Fifa utashirikisha mataifa 19 wanachama wa Fifa.