Kamati ya rufani ya Shirikisho la Soka Tanzania, TFF imetupilia mbali rufani iliyokatwa na aliyekuwa Makamu wa Rais wa shirikisho hilo Michael Wambura.
Wambura alifungiwa maisha kujihusisha na mchezo wa soka baada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ikiwemo kosa la kuishushia hadi TFF kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya rufaa ya maadili ya TFF, Ebenezer mashana amenukuliwa jana jijini Dar es salaam akisema adhabu ya Wambura ilikuwa sahihi kutokana na uzito wa makosa yaliyokuwa yakimkabili.
Tayari kamati ya utendaji ya TFF, ilimteua Athuman Nyamlani kukaimu nafasi ya makamu wa rais wa TFF wakati mchakato wa kumpata makamu wa rais ukiendelea.
Hata hivyo wakili wa Wambura, Emanuel Muga amesema anashangzwa na uamuzi uliofanywa na kamati ya rufani ya maadiuli na kwamba wataitafuta haki ya mteja wao mahali popote.