Na Fredrick Nwaka
Dar es Salaam. Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania umemalizika jioni hii ambapp Wallace Karia amechaguliwa kuwa rais mpya kwa kupata kura 95.
Karia alikuwa akipambana na wagombea wengine watano akiwemo Katibu Mkuu wa zamani wa TFF, Frederick Mwakalebela na mchezaji wa zamani wa Yanga, Ally Mayay.
Uchaguzi huo umemalizika jioni hii katika ukumbi wa St. Gasper uliopo mjini Dodoma.
Michael Wambura amechaguliwa kuwa makamu wa rais wa TFF baada kuwashinda wagombea wengine watano.
Wajumbe wa mkutano huo pia wamewachagua wajumbe wa kanda 13 za soka nchini Tanzania.
Rais aliyemaliza muda wake Jamal Malinzi alishindwa kuwania muhula wa pili kutokana na kushikiliwa na vyombo vya usalama akituhumiwa kwa makosa ya utakatishaji fedha.
Viongozi waliochaguliwa wameapishwa leo mjini Dodoma na wana Kazi ya kurejesha imani ya wapenda soka nchini Tanzania.