Connect with us

Benki ya Kenya, KCB, imetoa Shilingi za Tanzania 325,000,000 kufadhili ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa mwaka 2017/18.

Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo nchini Tanzania, Cosmas Kimario amesema Benki hiyo imejitokeza kufadhili soka nchini humo kwa sababu ya mafanikio ya ukuzaji soka inayoendelea kuonekana nchini humo.

Aidha, amesema kuwa wameamua kufadhili ligi hiyo kwa sababu michezo inaleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii ni pia chanzo cha ajira kwa vijana na burudani.

Tunajivunia kuwa benki rasmi ya VPL kwa Mwaka 2017/18,” amesema Kimario.

“Tunayo furaha kubwa kudhamini ligi Kuu Soka Tanzania Bara”. ameongezea.

Rais wa Shirikisho la soka nchini Tanzania Wallace Karia amesema kuwa, fedha hizo zitasaidia katika uimarishaji wa ligi kuu nchini humo na utasaidia kufadhili vlabu nchini humo.

TFF na KCB ni taasisi zenye mafanikio Benki imedumu kwa zaidi ya miaka 100 vivo hivyo mpira wa miguu nchini,” alisema Karia.

 

More in