Msimu wa ligi kuu ya soka nchini Uganda, mwaka 2016 unafika mwisho Ijumaa hii.
Tayari klabu ya KCCA imepata ubingwa wa ligi hiyo na watatawazwa mabingwa rasmi katika mchuano wake wa mwisho dhidi ya Sadolin Paints FC katika uwanja wa Nakivubo jijini Kampala.
Ratiba kamili ya michuano ya mwisho:
- KCCA FC Vs Sadolin Paints FC- Uwanja wa Nakivubo
-
Bright Stars FC Vs Soana FC, CS– Uwanja wa Matugga
-
JMC Hippos FC Vs Simba FC,-Uwanja wa Kakindu -Jinja
-
Lweza FC Vs Bul FC, -Uwanja wa Wankulukuku
-
Maroons Vs SC Villa ,-Uwanja wa Luzira Prison
-
Police FC Vs Express FC, -Uwanja wa Kavumba Recreational , Wakiso
-
The Saints FC Vs Vipers SC, -Uwanja wa Namboole Stadium
-
URA FC Vs SC Victoria University– Uwanja wa Mehta -Lugazi
KCCA ambayo ni klabu ya jiji kuu la Kampala, ilinyakua ubingwa baada ya kupata alama 56 alama nne mbele ya Vipers FC ambayo in alama 52 baada ya mechi 28.
Hii inamaanisha kuwa Vipers FC hawawezi kuifikia alama 56 hivi leo hata wakishinda mchuano wake wa leo.
Hili ni taji la 11 la KCCA tangu ilipoanza kushiriki ligi kuu ya soka nchini humo.
Klabu hii inayofahamika kwa jina maarufu “Kasasiro Boys” ilishinda ligi mara ya kwanza 1976.
Mwaka ujao itawaikilisha nchi hiyo katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika, michuano ambayo imeshiriki mara tatu.