Chama cha Jubilee kinasema mchezaji huyo wa zamani, ameaminiwa kwa sababu ya taibia yake na ushirikiano wake na watu.
Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya soka ya Kenya McDonald Mariga amekabidhiwa bendera ya chama cha Jubilee kuwania ubunge wa eneo bunge la Kibra jijini Nairob mwezi Novemba.
Mariga aliweka historia kwa kuwa mchezaji wa kwanza, raia wa Kenya kucheza katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya UEFA, wakati akichezea klabu ya Inter Milan nchini Italia mwaka 2010.
Aliwahi pia kucheza soka katika klabu ya Parma huko Italia.
Mbali na Italia, aliwahi pia kucheza soka nchini Uhsipania katika klabu ya Real Sociedad na Real Oviedo.
Alianza kuichezea Harambee Stars mwaka 2003 na kwa mech 40 alizicheza, alifunga mabao 5.