-
-
by
Victor Abuso
Timu ya taifa ya soka ya Kenya Harambee Stars imepata ushindi wa bao 1 kwa 0 dhidi ya Cape Verde katika mchuano muhimu kutafuta tiketi ya kufuzu katika fainali ya kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Bao pekee la Stars lilitiwa kimyani na mshambuliaji matata Michael Olunga katika kipindi cha kwanza cha mchuano huo uliochezwa katika uwanja wa taifa wa Nyayo jijini Nairobi.
Ushindi huo ni muhimu kwa Kenya ambayo itarudiana na Cape Verde ugenini mapema juma lijalo na mshindi atafuzu katika hatua ya makundi kuendelea katika hatua ya kusaka tiketi kwenda Urusi.
Kipindi cha kwanza cha mchuano huo kilitawaliwa na Kenya ambayo ilikuwa inafanya mashambulizi yalioongozwa na Olunga na mwenzake Johana Omollo huku wakisaidiwa na nahodha Victor Wanyama aliyetawala safu ya kati.
Cape Verde ilibadilika kipindi cha pili kwa kujitahidi kupiga mashuti lakini kipa wa Kenya Boniface Oluoch alionekana macho langoni.
Kenya imekuwa ikiifuga Cape Verde alimaarufu kama Blue Sharks kuanzia mwaka 2002.



Africa Cup of Nations
Teams get tough opponents in AFCON 2025 Draws

Africa Cup of Nations
Tanzania,Uganda in tricky group with Nigeria and Tunisia

Africa Cup of Nations
Tough Afcon Group B as SouthAfrica paired with Egypt,Angola,Zimbabwe

Africa Cup of Nations
Teams get tough opponents in AFCON 2025 Draws

Africa Cup of Nations
Tanzania,Uganda in tricky group with Nigeria and Tunisia

Africa Cup of Nations
Tough Afcon Group B as SouthAfrica paired with Egypt,Angola,Zimbabwe
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...