Timu ya taifa ya soka ya Kenya, inahitaji siku ya Jumapili dhidi ya Ethiopia kujiweka katika sehemu nzuri ya kufuzu katika fainali ya bara Afrika AFCON mwaka 2019 nchini Cameroon.
Mechi hiyo itakuja baada ya nchi hizo mbili kukutana katika mchuano wa kwanza siku ya Jumatano jijini Addis Ababa na Kenya kulazimisha sare ya kutofungana.
Matokeo haya yameonekana kuwa mazuri kwa Kenya ambayo inaongoza kundi la F, nyuma ya Ethiopia ambayo pia ina alama nne.
Ghana ni ya tatu kwa alama tatu, huku Sierra Leone ikiwa imefungiwa na Shirikisho la soka duniani FIFA kwa muda usiojulikana kujihusisha na masuala ya soka.
Ethiopia pia ina nafasi ya kufuzu iwapo, itapata alama tatu muhimu dhidi ya Harambee Stars jijini Nairobi huku kocha wa nchi hiyo Abraham Mebartu akisema mechi hiyo itaamua hatima yao.
Kenya itamaliza mechi yake ya mwisho dhidi ya Ghana, mwezi Machi mwaka 2019 huku Ethiopia ikimalizia kibarua chake dhidi ya Ghana mwezi Novemba.
Mataifa 24 yatafuzu kushiriki katika mashindano ya mwakani, kutoka mataifa 16.
Mechi hizo za kufuzu zinaendelea:-
Alhamisi Oktoba 11 2018
Congo vs Liberia
Ijumaa Oktoba 12 2018
Cameroon vs Malawi
Gabon vs Sudan Kusini
Angola vs Mauritania
Nigeria vs Libya
Guinea vs Rwanda
Cote d’Ivore vs Jamhuri ya Afrika ya Kati
Misri vs Swaziland
Cape Verde vs Tanzania
Togo vs Gambia
Mali vs Burundi
Algeria vs Benin