Connect with us

 

Leo ni siku ya mapumziko ya katika michuano ya soka kuwania ubingwa barani Afrika kwa upande wa wanawake.

Mechi hizi zitarejelewa kesho, wakati michuano ya kundi A zitafikia mwisho jijini Yaoude nchini Cameroon.

Zimbabwe itakabiliana na Cameroon huku Misri ikicheza na Afrika Kusini mechi ambazo zitachezwa kwa wakati mmoja kuanzia saa 12 jioni saa za Afrika Mashariki.

Wenyeji Cameroon wameshafuzu katika hatua ya mwondoano baada ya kushinda mechi mbili za kwanza, lakini Misri ambayo ina alama tatu, Afrika Kusini na Zimbabwe ambazo zina alama moja zinahitaji kushinda ili kusonga mbele.

Hata hivyo katika kundi B, matumaini ya Kenya ambayo inashiriki kwa mara ya kwanza katika michuano hii yametoweka baada ya kushindwa michuano yote miwili. Siku ya Jumatano jioni, Kenya ilifungwa na Mali mabao 3-1.

Kundi hili linaongozowa na mabingwa watetezi Nigeria ambao wana alama 4 sawa na Ghana ambao wanashikilia nafasi ya pili.Mali nao wana alama tatu na wahitaji ushindi dhidi ya Ghana ili kufuzu.

Mechi za mwisho za kundi B zitachezwa siku ya Jumamosi, kuanzia saa tatu usiku saa za Afrika Mashariki.

Ratiba

Mali vs Ghana

Kenya vs Nigeria

More in AWCON