Connect with us

 

Shirikisho la soka duniani FIFA, limetoa orodha ya mataifa bora duniani kwa mwezi Juni.

Katika ukanda wa Afrika Mashariki, Harambee Stars ya Kenya imepanda kwa nafasi 43 na sasa ni ya 86 duniani.

Taifa Stars ya Tanzania, imepanda kwa nafasi 13 na sasa ni 123 duniani.

Uganda ambayo inaendelea kuwa nchi bora Afrika Mashariki, imepanda kwa nafasi tatu na sasa ni ya 69, huku Burundi ikipanda nafasi 7 na Sudan Kusini ikipanda kwa nafasi 4.

Hata hivyo, Sudan imeshuka nafasi 14 na kufikia nafasi ya 142 ikifuatwa na Rwanda ambayo imeshuka nafasi 8 na sasa ni ya 111, huku Ethiopia nayo ikiwa ya 132 baada ya kushuka nafasi 7.

Orodha katika nchi za Afrika Mashariki

1. Uganda (69)
2. Kenya (86)
3. Rwanda (111)
4. Tanzania (123)
5. Burundi (125)
6. Ethiopia (132)
7. Sudan (142)
8. South Sudan (153)
9. Djibouti (205)
10. Eritrea (205)
11. Somalia (205)

Orodha barani Afrika

1 Algeria
2 Ivory Coast
3 Ghana
4 Senegal
5 Egypt
6 Tunisia
7 Cameroon
8 Morocco
9 Congo DR
10 Mali

More in