Na Fadhili Sizya
Kipa mkongwe Ivo Mapunda ametangaza kusaka klabu ya kucheza soka kutoka nje ya nchi baada ya kutumikia kwa muda mrefu katika soka la Tanzania.
Akizungumza katika mahojiano maalum na soka25east.com,alisema kuwa tayari anao uzoefu mkubwa kucheza soka la nyumbani hivyo anafikiri nafasi kubwa ya kuendelea kufanya vizuri ataipata ikiwa atacheza soka la kulipwa.
Aidha kipa huyo alisema kwa sasa anacho kituo cha kulelea vijana wa soka (football academy) ambapo yupo katika mipango ya kukiimarisha huku akijipanga na yeye kuendelea binafsi.
Pia Mapunda alithibitisha kufuta uvumi wa kutangaza kustaafu na ukimya wake katika soka ni kujipanga katika soka la kulipwa.
Hata hivyo Mapunda aliwahi kucheza klabu za Yanga, Moro United, Simba Sc, African Lyon, Azam Fc na nje ya Tanzania aliwahi kucheza Gor Mahia, St George na kuwa kulitumia taifa la Tanzania akiwa kipa namba moja