Connect with us

Vlabu vya Afrika Mashariki vinarejea uwanjani mwishoni mwa juma hili, kucheza mechi ya marudiano kutafuta nafasi ya kufuzu katika hatua ya makundi, kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika mwaka 2017.

Zanaco ya Zambia itakuwa nyumbani kumenyana na Yanga FC ya Tanzania jijini Lusaka siku ya Jumamosi jioni.

Mchuano wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam wiki iliyopita, vlabu vyote viwili vilitoka sare ya kufungana bao 1-1 katika uwanja wa Taifa.

Mabingwa wa soka nchini Zambia wanashiriki katika michuano hii mara 7 huku Yanga ikishiriki katika michuano hii mara 11, wakati huu kila timu ikitaka kusonga mbele na kushinda taji hili.

Yanga inakwenda katika mchuano huu ikiwa na historia ya kufika katika mzunguko wa pili msimu uliopita, baada ya kuondolewa na Al Ahly ya Misri.

Mwaka 2010, Zanaco pia ilifika katika mzunguko wa pili wa michuano hii mikubwa barani Afrika.

Kazi kubwa ni kwa Yanga ambao wapo chini kwa bao moja kutoka na bao la ugenini la Zanaco.

Pamoja na hilo, kocha wa Yanga George Lwandamina ambaye ni raia wa Gambia atakuwa anataka kupata ushindi nyumbani lakini pia kuendelea kulinda kibarua chake.

Mbali na mchuano huu, mabingwa watetezi Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini itakuwa jijini Kampala kumenyana na KCCA.

Mchuano wa mzunguko wa kwanza, mabingwa watetezi walishinda kwa mabao 2-1 na kuwaweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele katika hatua ya makundi.

Siku ya Jumapili, TP Mazembe ya DRC itakuwa ugenini kucheza na CnaPS United ya Zimbabwe.

AC Leopard ya Congo Brazavile itachuana na Saint George ya Ethiopia huku, Gambia Ports Authority ikiwa ugenini kupambana na AS Vita Club.

More in East Africa