Na Mwandishi wetu akiwa Dar Es Salaam,
Baada ya maneno ya baadhi ya watu kuwa mengi kuhusiana na kiwango cha Mbwana Samatta alichokionesha katika mchezo wa Tanzania dhidi ya Libya nchini Tunisia, kiasi cha Tanzania kupoteza mchezo huo 2-1 Libya ikitokea nyuma.
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Etienne Ndairagije raia wa Burundi ameeleza na kujibu tuhuma za baadhi ya mashabiki kwa kueleza kuwa sio sawa kulinganisha kiwango cha Samatta akiwa Genk na Taifa Stars, kwa sababu Genk wanacheza mfumo ulioundwa kumzunguuka Samatta wakati Tanzania timu ndio kwanza mpya na anaunda mfumo.
“hilo ni jambo ambalo linatokea sana mara nyingi hata mitandaoni utasikia Messi wanamkosoa hivyo hivyo, Salah na Mane pia wanamuona Liverpool wanataka wamuone tena Senegal hilo ni jambo la kawaida kwa watu kuliongelea”
“Sisi tubadilike tumpe moyo (Samatta) aendelee kuwa nasi kuwepo kwake anatusaidia na kujitolea zaidi tuendelee kumtia moyo ili aendelee kuwa bora zaidi”
“Naweza kulizungumzia kidogo Genk ana muda mwingi kwa hiyo timu ya Genk imejengeka kupitia kwake, timu yetu ambayo tunaijenga tutafute namna anavyoweza kucheza (Samatta) wachezaji ambao yupo nao Genk sio hawa ambao yuko nao huku, mashindanoo anayocheza kule sio anayocheza huku, viwanja anavyocheza kule sio anavyocheza huku kwa hiyo ni vitu tofauti muache kulinganisha”
Tanzania sasa ipo nafasi ya tatu katika msimamo wa Kundi J ikiwa na alama 3, Libya nafasi ya pili kwa kuwa na alama 3, Tunisia akiongoza Kundi hilo kwa kuwa na alama 6 huku Equatorial Guinea kwa sasa akiwa mnyonge wa Kundi kwa kuwa na alama 0.
CAF Champions League
Mamelodi Sundowns and Asfar advance to Quarter-finals
CAF Champions League
TP Mazembe bow out with big win over leaders Al Hilal
CAF Champions League
MC Alger book Quarter-finals spot after draw with Yanga
CAF Champions League
Orlando Pirates capped their incredible with Al Ahly win
Women's Football
FAZ appoints Hauptle as new Copper Queens Coach
Africa Cup of Nations
CAF Slaps Libya with $50,000 fine, Benin also sanctioned
CAF Champions League
Raja Casablanca upset Mamelodi Sundowns
CAF Champions League
Mouth Watering CAF Champions League matches lined up
CAF Champions League
Al Ahly, Al Hilal Omdurman and Esperance looking to book Quarter-finals slot
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...