Mshabuliaji wa klabu ya soka ya Barcelona Luis Suarez ameifikisha timu yake katika fainali ya kombe la dunia baina ya vilabu baada ya kuifungia mabao 3 kwa 0 dhidi ya Guangzhou Evergrande FC ya China katika hatua ya nusu fainali siku ya Alhamisi.
Barcelona ya Uhispania sasa itamenyana na River Plate FC ya Argentina siku ya Jumapili mjini Yokohama nchini Japan katika fainali ya mwaka huu.
Baada ya kushinda mechi hiyo, kocha wa Barcelona Luis Enrique amemsifia Suarez na kumwelezea kama mchezaji bora na hatari mbele ya lango la mpinzani.
Mabingwa hawa wa soka barani Ulaya, walicheza mchezo huo wa nusu fainali bila ya mshambuliaji wao wa kutegemewa Lionel Messi ambaye anasumbuliwa na maradhi na figo na huenda atakosa mechi ya fainali .
Naye kocha wa Guangzhou Evergrande FC Luiz Felipe Scolari amewashukuru wachezaji wake kwa kuonesha kiwango kizuri katika mashindano hayo licha ya kufungwa katika hatua ya nusu fainali.
Barcelona walishinda taji hili la kombe la dunia baina ya vlabu mwaka 2009 na 2011.
Real Madrid ya Uhispania walioshinda taji la mwaka 2014 wkaati michuano hii ilipoandaliwa nchini Morroco, waliondolewa katika mashindano haya.