Na Victor Abuso
Mataifa manne ya Afrika yamefuzu katika hatua ya 16 bora katika michuano ya dunia ya mchezo wa soka baina ya vijana wasiozidi umri wa miaka 20 inayoendelea nchini New Zealand.
Nigeria, Ghana, Mali na Senegal zimefuzu baada ya kufanya vizuri katika michuano ya makundi.
Ghana itamenyana na Mali, Nigeria dhidi ya Ujerumani huku Senegal ikipambana na Ukraine.
Michuano hii ya mwodoano itaanza Juni tarehe 10 huku mchuano wa kwanza ukiwa kati ya timu kutoka barani Afrika Mali dhidi ya Ghana.
Ghana ilimaliza ya kwanza katika kundi lake kwa alama 7, baada ya kushinda michuano miwili na kwenda sare mchuano mmoja bila ya kupoteza mchuano wowote.
Mali nayo ilipata ushindi wa bao 1, ikatoka sare mchuano mwingine na kupoteza mchuano wake wa tatu.
The Flying Eagles ya Nigeria ilifuzu katika hatua hiyo baada ya kushinda mchuano wake wa mwisho dhidi ya Hungary baada ya kuwashinda mabao 2 kwa 0 na kufuzu pamoja na Brazil katika kundi hilo.
Senegal nayo ilipata ushindi mmoja, kutoka sare mechi moja na kufungwa mechi moja.
Mataifa yote ya Afrika yanalenga kufanya vizuri na angalau mojawpao kufika fainali na kushinda taji hili na kuwa taifa la pili baada ya Ghana kunyakua taji hili kama ilivyokuwa mwaka 2009 wakati michuano hii ilipoandaliwa nchini Misri.
Ratiba kamili:-
Brazil vs Uruguay
Portugal vs New Zealand
Austria vs Uzbekistan
Ukraine vs Senegal
United States of America vs Colombia
Serbia vs Hungary
Ghana vs Mali
Germany vs Nigeria
Mechi ya fainali itachezwa tarehe 20 mwezi Juni mjini Auckland.