Kongamano la 66 la Shirikisho la soka duniani FIFA linafanyika mwishoni mwa wiki hili mjini Mexico nchini Mexico.
Llitakuwa kongamano la kwanza kuongozwa na rais mpya wa FIFA Gianni Infantino, aliyechaguliwa mwezi Februari mwaka huu.
Ni kongamano la kwanza pia tangu kubadilishwa kwa kanuni muhimu za FIFA kuhusu watakaohudumu katika Kamati ya utendaji ya Shirikisho la soka FIFA.
Miongoni mwa mabadiliko hayo ni pamoja na kuwa na Mwanamke katika Kamati hiyo juu ya FIFA .
Mwezi Aprili, ilikubaliwa pia kuwa kufikia mwisho wa mwezi Septemba mwaka huu, Mashirikisho ya mabara duniani yawe yamekubaliana kuhusu watakaowawakilisha katika Kamati kuu ya FIFA.
Hii ndio mara ya kwanza, kongamano la FIFA linalohudhuriwa na viongozi wa Mashirkisho yote duniani 209 linafanyika nchini Mexico baada ya michuano ya kombe la dunia mwaka 1986.
Rais Infatino anasema kongamano hilo litatumiwa kuweka mikakati ya kuinua mchezo wa soka lakini pia wadau wa soka watabadilishana mawazo kuhusu namna ya kuimarisha mchezo huu unaopendwa duniani.
Kabla ya mkutano wa Ijumaa, mashirikisho ya soka CAF, CONCACAF, CONMEBOL, OFC na AFC yatakuwa na vikao vyake.