Na Victor Abuso
Tusker FC na KCB zimepata ushindi katika michuano yao ya ligi kuu ya Kenya KPL iliyochezwa siku ya Jumamosi.
Baada ya kipindi kirefu, Kocha wa Tusker FC Francis Kimanzi alionekana mwenye furaha baada ya vijana wake kuwafunga wanasukari Sony Sugar mabao 2 kwa 0 katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa Kimataifa wa Kasarani jijini Nairobi.
Matokeo mabaya ya Sony Sugar yanaweka hatarini kibarua cha kocha Zedekiah Otieno ambaye inavyoonekana kibarua chake huenda kikaota nyasi ikiwa hali itaendelea kumwendea vibaya.
Ushindi wa Tusker unaiweka katika nafasi ya tano katika msururu wa ligi kwa alama 22 sawa na Thika United ambayo itakabiliana na viongozi wa ligi na mabingwa watetezi Gor Mahia siku ya Jumatatu.
Sony Sugar kutoka mitaa ya Awendo, nayo ipo katika nafasi ya 11 kwa alama 15.
Vikosi vya timu zote mbili.
Tusker: 20. Faruk Shikalo, 5. Joackins Atudo, 2. James Situma, 15. Donald Mosoti, 17. Lloyd Wahome, 8. Brian Osumba, 10. Kevin Kimani, 30. Humphrey Mieno, 14. Jesse Were, Daniel Oyirwoth, 60’ Dennis Nzomo) 16. Patrick Onyango (76’ Abud Omar)
Wachezaji wa akiba : 29. Bryne Omondi (GK), 23. Steven Owusu 26. Mathew Odongo 11. Ismail Dunga, 18. Clifford Alwanga
Sony Sugar : 22. Jairus Adira (GK) 23. Byron Odiaga (49’ Wycliffe Nyangech) 3. Samuel Olare, 17. Joseph Omweri, 26. Alfred Onyango, 9. Amos Asembeka, (73’ Okombo Naftali) 4. Kennedy Odour, 19. Edwin Odour, 21. Samuel Onyango, 20. Ademba Victor 11. Ogutu Vincent (63’ Meshack Muyonga)
Wachezaji wa akiba: 35. Kevin Omondi (GK), 7. Marwa Chamberi, 16. Nicholas Akoko, 6. Victor Ayugi,
Katika matokeo mengine, KCB walipata ushindi mkubwa baada ya kuwachabanga Muhoroni Youth mabao 3 kwa 0 mchuano ambao pia ulichezwa katika uwanja wa Kasarani jijini Nairobi.
Chemelil Sugar walitoka sare ya kutofungana na Western Stima huku City Stars nao wakiwa nyumbani wakiambulia sare ya bao 1 kwa 1 na Nakuru All Stars.
Siku ya Jumapili, Sofapaka FC wanaofahamika kwa jina maarufu kama Batoto Ba Mungu watachukuana na wanajeshi Ulinzi Stars jijini Nairobi.
Siku ya Jumatatu ambayo itakuwa ni Sikukuu ya Madaraka, Ushuru watapambana na Bandari FC , Mathare United na AFC Leopards lakini pia mabingwa watetezi Gor Mahia watachuana na wenyeji wao Thika United.