Connect with us

Ligue 1: Benjamin Moukandjo awaongoza waafrika kufunga mabao

Ligue 1: Benjamin Moukandjo awaongoza waafrika kufunga mabao

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Cameroon, Benjamin Moukandjo anaongoza wachezaji wenzake kutoka barani Afrika katika safu ya ufungaji wa mabao katika ligi kuu ya soka nchini Ufaransa Ligue 1 inayokamilika mwishoni mwa juma hili.

Moukandjo ambaye amekuwa akiichezea klabu yake ya Lorient, ameisaidia klabu yake kutoshushwa daraja kwa kuipa mabao 12 baada ya kucheza michuano 25.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, alijiunga na Lorient akitokea klabu nyingine ya Ufaransa ya Reims mwaka uliopita.

Kiungo wa kati wa Kimataifa wa Lille Morroco Sofiane Boufal naye anashikilia nafasi ya pili kwa mabao 11.

Pamoja na hilo, Boufal alitajwa kuwa mchezaji wa Afrika aliyeshinda taji la mwaka huu la mchezaji wa zamani wa Cameroon Marc-Vivien Foe aliyefariki dunia akiwa uwanjani mwaka 2003.

Mchezaji mwingine kutoka barani Afrika, Abdul Majjed Waris raia wa Ghana anayechezea pia klabu ya Lorient, naye ameifungia klabu yake mabao 11, huku Cheick Diabaté kutoka Mali akiifungia timu yake ya Bordeaux mabao 10.

Mabingwa wa ligi kuu ya soka nchini humo msimu huu ni Paris Saint-Germain na mshambuliaji wake matata Zlatan Ibrahimovic raia wa Sweden amefunga mabao 35.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in