Mechi za ligi kuu ya soka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zinarejelewa tena baada ya kuahirishwa kwa sababu ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwisho wa mwezi wa Desemba mwaka 2018.
Klabu ya Groupe Bazano yenye makao yake mjini Lubumbashi, inayoshikilia nafasi ya 10 katika msururu wa ligi kuu kwa alama 13, siku ya Alhamisi itamenyana na DC Motema Pembe.
Mechi hii itachezwa katika uwanja wa Frederic Kibassa Maliba mjini Lubumbashi.
Baada ya mechi Alhamisi, Groupe Bazano itakuwa na kibarua kingine nyumbani mwishoni mwa wiki dhidi ya AS Vita Club ya Kinshasa, kabla ya kusafiri kwenda kumenyana na Maniema Union katikati ya wiki ijayo.
Mechi zingine za siku ya Alhamisi, Januari 03 2019:-
Nyuki vs Renaissance
Don Bosco vs Vita Club
Ijumaa, Januari 04 2019
Mont Bleu vs Rangers
Maniema Union vs Motema Pembe
Jumapili, Januari 06 2018
Dauphins Noirs vs Nyuki
Don Bosco vs Motema Pembe
Groupe Bazano vs Vita Club
Ligi hiyo inaongozwa na TP Mazembe ambyo ina alama 40, baada ya mechi 15, ikifuatwa na Vita Club ambayo baada ya mechi 11 ina alama 28.