Connect with us

 

Mashabiki wa ligi kuu nchini Kenya, mwishoni mwa wiki hii wanalazimika kufurika katika viwanja mbalimbali nchini humo kutazama mechi za ligi kuu baada ya Runinga ya Supersport iliyokuwa inaonesha mechi hizo kuvunja mkataba wake na kampuni inayosimamia ligi kuu KPL wiki mbili zilizopita.

Supersport ilisema iliamua kuondoka baada ya kusema kuwa haifahamu kati ya KPL na Shirikisho la soka FKF.

FKF iliamua msimu huu uwe na vlabu 18 huku KPL ikitaka 16, uamuzi ambao umewakasirisha wafadhili hao.

Rais wa FKF Nick Mwendwa amekuwa akifanya mazungumzo wiki hii na wadau mbalimbali wa soka nchini humo kujaribu kuangalia uwezekano wa kurejea kwa wafadhili hao, lakini haijafahamika ni lini mwafaka utapatikana.

Hata hivyo, ratiba ya michuano ya ligi kuu inaendelea kama kawaida.

Wachambuzi wa soka nchini Kenya, wanaona kuwa baada ya kuondoka kwa wafadhili hao huenda msisimko wa michuano ya ligi kuu ukashuka sana .

Mabingwa wa zamani Gor Mahia, wanaongoza kwa alama 9 baada ya mechi nne, wakifuatwa na Posta Rangers ambao wana alama 8.

Ratiba Jumamosi Aprili 15 2017

Sony Sugar vs Gor Mahia

Tusker FC vs Ulinzi Stars

Ratiba Jumapili Aprili 16 2017

Bandari vs Thika United

AFC Leopards vs Muhoroni Youth

Kakamega Homeboyz vs Nzoia United

Western Stima vs Chemelil Sugar

Zoo Kericho vs Sofapaka

Ratiba ya Jumatatu Aprili 17 2017

Kariobangi Sharks vs Nakumatt

Mathare United vs Posta Rangers

More in