Connect with us

Ligi ya Zanzibar yasimamishwa kutokana na mzozo wa uongozi

Ligi ya Zanzibar yasimamishwa kutokana na mzozo wa uongozi

Mahakama Visiwani Zanzibar nchini Tanzania imeagiza ligi kuu ya soka visiwani humo kusimamishwa kutokana na Shirikisho la soka ZFA kukabiliwa na kesi mbalimbali.

Uamuzi huu umeweka njia panda ligi kuu ya soka Visiwani humo iliyoratibiwa kuanza mwezi Septemba na haijulikani ni lini suluhu itapatikana.

Shirikisho la soka la Zanzibar ZFA kwa muda mrefu limekuwa likikabiliwa na matatizo ya uongozi na hata kuwa na zaidi ya katiba moja inayosimamia mchezo huu wa kandanda.

Moja ya kesi iliyofunguliwa na Naibu rais wa ZFA Unguja Haji Ameir Haji, inawakabili viongozi wa juu wa shirikisho hilo akiwemo kiongozi wa ZFA, Ravia Idarous Faina, Makamu wa Rais ZFA Pemba, Ali Mohamed Ali na Katibu Mkuu wa ZFA, Kassim Haji Salum.

Kesi hiyo inalalamikia ukiukwaji wa utaratibu wa kuifanyia marekebisho katiba ya Shirikisho hilo, tuhma za matumizi mabaya ya fedha na pia maswala ya ubaguzi katika uongozi huo.

Pamoja na kesi hiyo klabu ya Chuoni kwenda Mahakamani kupinga kushushwa daraja ya kushiriki ligi kuu msimu huu.

Wachambuzi wa soka wanasema mzozo huu ukiendelea huenda soka la Zanzibar likaendelea kudidimia.

 

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in