Ligue 1 ndio ligi ya juu ya wachezaji wa kulipwa nchini Ufaransa.
Ligi hiyo ilianza mwezi Septemba mwaka 1932 wakati huo ikiitwa ligi ya taifa, baadaye ikabadilishwa jina na kufahamika ligi ya daraja la kwanza.Kuanzia mwaka 2002 jina lilibadilishwa tena hadi Ligue 1.
Timu zinazoshiriki katika ligi hii kila msimu ni 20.
Msimu mpya huwa unaanza mwezi Agosti na kumalizika mwezi Mei. Timu tatu hupandishwa daraja na zingine tatu zikishushwa daraja.
Kila timu hucheza mechi 38 huku idadi ya mechi zinazochezwa zikiwa 380 kila msimu.
Idadi kubwa ya mechi huchezwa mwishoni mwa juma, Jumamosi na Jumapili.
Ligi husitishwa kwa wiki mbili kuelekea Sikukuu ya Krismasi na hurejelewa tena katika wiki ya pili baada ya mwaka mpya.
Ligue1 inaorodheswa ya tano katika orodha ya ligi bora duniani, nyuma ya La Liga ya Uhispania, Ligi kuu ya Uingereza, Bundesliga ya Ujerumani na Seria A ya Italia.
Klabu ya Saint-Ettiene ndio klabu iliyofanikiwa sana katika historia ya ligi hiyo kwa kushinda mataji 10 mwisho ikiwa ni msimu wa mwaka 1980/1.
Olmpique Lyon nayo inaingia katika vitabu vya historia kwa kuwa klabu ambayo imeshinda mataji saba mfululizo kati ya mwaka 2002 hadi 2008.
FC Sochaux na Olmpique de Marseille ndio timu mbili ambazo zimeshiriki katika misimu mingi huku FC Nantes ikishiriki katika misimu 44 bila kushushwa daraja kati ya mwaka 1963-2007.
Mabingwa wa mwaka 2015/6 ni Paris Saint-Germain na hili ni taji lao la 6.