Luka Modric, kiungo wa kati anayechezea klabu ya Real Madrid nchini Uhispania na timu ya taifa ya Croatia, ndio mchezaji bora wa mwaka 2018.
Modric alishinda tuzo hiyo baada ya kumshinda Cristiano Ronaldo anayechezea klabu ya Juventus na Mohammed Salah kutoka Misri anayechezea klabu ya Liverpool nchini Uingereza aliyeshinda, tuzo ya bao bora la mwaka 2018.
Mchezaji huyo wa Croatia aliisaidia timu yake kufika katika hatua ya fainali ya kombe la dunia licha ya kushindwa na Ufaransa mwezi Julai, lakini pia aliisaidia klabu yake kushinda taji la klabu bingwa barani Ulaya.
Tuzo ya mwaka 2018 ilitolewa katika hafla iliyofanyika jijini London nchini Uingereza Jumatatu usiku.
Kuanzia mwaka 2017 tuzo la FIFA limekuwa likitolewa kwa ushirikiano na lile la Ufaransa la Ballon d’Or na siku hizi hufahamika kama FIFA Ballon d’Or, ushirikiano ambao utaendelea kwa miaka sita.
Orodha kamili ya washindi:
Bao bora la mwaka
Mohamed Salah (Misri & Liverpool)
Kocha bora wa mwaka kwa upande wa wanaume
Didier Deschamps (Ufaransa)
Kipa bora
Thibaut Courtois (Ubelgiji & Real Madrid)
Kocha bora kwa upande wa wanawake
Reynald Pedros (Lyon)
Shabiki bora wa mwaka
Mashabiki kutoka Peru, wakati wa kombe la dunia nchini Urusi.
Mchezajimwenye nidhamu
Lennart Thy (Ujerumani)
Kikosi bora cha wachezaji 11 duniani
David De Gea, Dani Alves, Raphael Varane, Sergio Ramos, Marcelo, Luka Modric, N’Golo Kante, Eden Hazard, Lionel Messi, Kylian Mbappe, Cristiano Ronaldo
Mchezaji bora kwa upande wa wanawake
Marta (Orlando Pride & Brazil)
Mchezaji bora kwa upande wa wanaume
Luka Modric (Croatia & Real Madrid)