Connect with us

Lweza yaendelea kupanda ligi kuu ya soka nchini Uganda

Lweza yaendelea kupanda ligi kuu ya soka nchini Uganda

Klabu ya soka ya Lweza FC nchini Uganda iliilemea Saints FC mabao 2 kwa 0 katika mchuano wa ligi kuu ya soka nchini humo.

Mchuano huo ulichezwa Jumanne jioni katika uwanja wa Mutesa II katika eneo la Wankulukuku jijini Kampala.

Mabao yote ya Lweza FC yalitiwa kimyani na Juma Balinya na Geoffrey Sserunkuma katika kipindi cha kwanza cha mchuano huo.

Vijana wa Lweza FC walionekana bora katika mchuano huo huku wachezaji Paddy Muhumuza na Emmanuel Kalyowa wakitawala safu ya mchuano huo.

Ushindi huu, umewafikisha Lweza FC katika nafasi ya 9 ikiwa na alama 30 huku Saints FC ikisalia katika nafasi ya 13 kwa alama 19 baada ya michuano 20 kuchezwa.

Wachezaji:

Lweza FC: Charles Lukwago (G.K), Fred Okot, Nestroy Kizito, Michael Kabanda, Ibrahim Kiyemba, Ayub Kisaliita, Paddy Muhumuza, Moses Ndawula (81’Mustapha Kiragga ), Geofrey Sserunkuma (71′ Rajab Kakooza), Sula Bagala, Juma Balinya (75′ John Kisakye)

The Saints F.C : Yasin Mugabi (G.K), Fred Agandu, Hassan Musana, Marlon Tangawuzi, Bernard Agele, Fahad Kawooya, Ivan Kiweewa (57’Eric Sebuguzi, ), Isaac Kirabira, Yasin Mugume, Patrick Senfuka (39′ George Ssenkaaba), Alex Kitata (70′ Nicolas Odong)

Matokeo Kamili:-

  • Bright Stars FC 1-2 KCCA FC
  • BUL FC 2-0 Express FC
  • Lweza FC 2-0 The Saints FC
  • Maroons FC 1-1 JMC Hippos FC 
  • SC VU 0-3 Sadolin Paints FC
  • URA FC 3-2 Simba FC 
  • Police FC 0-0 Vipers SC

More in