Na Mwandishi wetu akiwa Dar Es Salaam,
Toka Februari 2019 aliyekuwa makamu wa Rais wa shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) Michael Richard Wambura alikuwa anashikiliwa na Polisi na kuwa rumande kwa muda wote huo.
Wambura alikuwa anashikiliwa kwa makosa 17 ikiwemo kugushi nyaraka, uhujumu uchumi na utakatishaji fedha wakati akiwa kiongozi wa TFF makosa ambayo hayakuwa na dhamana.
Baada ya huruma ya Rais wa Tanzania kwa watuhumiwa wa makosa ya utakatishaji fedha na uhujumu uchumi kumuagiza muendesha mashtaka DPP wasamehe wale watuhumiwa watakaokiri kosa na kurudisha pesa watasamehewa.
Oktoba 7 Wambura ameachiwa huru katika Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu chini ya hakimu Kelvin Mhina baada ya kukubali kurejesha kwa awamu kiasi cha Tsh milioni 100 ($ 43,519) alichokuwa anatuhumiwa nacho toka Februari 11 2019 alipofikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza, Wambura ameanza kwa kulipa Tsh milioni 20 ($ 8,703) kama sehemu ya malipo ya awamu tano ya pesa hizo.