-
-
by
Victor Abuso
Mchezaji wa Kimataifa wa Kenya anayecheza soka la kulipwa katika ligi ya Serie B nchini Italia McDonald Mariga amefungiwa kutocheza michuano mitano baada ya kumsalimu kwa nguvu mwamuzi hadi akatoka damu mkononi.
Mariga anayechezea klabu ya Latina aliondolewa uwanjani kipindi cha pili wakati wa mchuano na klabu ya Virtus Entella na kwenda kumpa mkono mwamuzi kabla ya kuondoka uwanjani.
Kiungo huyo wa kati aliyewahi kuichezea klabu ya Inter Milan, Parma, Real Sociedad na Helsingborgs IF amepatikana na kosa lingine la kumtamkia maneno makali mwamuzi huyo.
Adhabu hii ya Kamati ya nidhamu inamaanisha kuwa Mariga mwenye umri wa miaka 29 hatoshiriki katika michuano inayosalia kabla ya msimu kumalizika.
Mariga alijiunga na klabu hiyo mwezi Januari na ameichezea mara 13 na kwa sababu ya adhabu hiyo atakosa mchuano muhimu dhidi ya Spezia siku ya Jumamosi.
Ni kaka yake Victor Wanyama anayechezea klabu ya Soutmptom nchini Uingereza.



Africa Cup of Nations
Teams get tough opponents in AFCON 2025 Draws

Africa Cup of Nations
Tanzania,Uganda in tricky group with Nigeria and Tunisia

Africa Cup of Nations
Tough Afcon Group B as SouthAfrica paired with Egypt,Angola,Zimbabwe

Africa Cup of Nations
Teams get tough opponents in AFCON 2025 Draws

Africa Cup of Nations
Tanzania,Uganda in tricky group with Nigeria and Tunisia

Africa Cup of Nations
Tough Afcon Group B as SouthAfrica paired with Egypt,Angola,Zimbabwe
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...