-
by
Victor Abuso
Mashabiki wa vlabu vya soka Yanga FC na Simba FC wamenza kurushiana maneno ya kishabiki siku mbili kabla ya mchuano muhimu wa watani wa jadi katika ligi kuu ya Tanzania bara kesho Jumamosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kila upande unavutia upande wake ukiwa na matumaini ya kupata ushindi.
Shaban Abdala mkaazi wa Magomeni, shabiki wa Yanga au maarufu vijana wa Jangwani amesema,
“Jumamosi hii hawatuwezi, tutawafunga tatu bila,” alisisitiza.
“Ni kweli katika siku za hivi karibuni wamekuwa wakitufunga lakini ya kale yamepita, msema kweli atajulikana Jumamosi,”. Aliongeza.
Sabina Martha mkaazi wa Tabata na shabiki wa Simba aliamaarufu Wekudu wa Msimbazi yeye anasema, Jumamosi klabu yake itaendeleza ubabe dhidi ya Yanga.
“Wajua tumezoea kuwashinda hawa watani wetu, wakati ule ilikuwa tano bila, wakati mwingine 3 bila na Jumamosi najua itakuwa tano bila,” alisisitiza.
Katika mitandao ya kijamii, hivi ndivyo ilivyoandikwa kuelekea mchuano huo, Angurumaaaapo Simba Mcheza nani..? ANGURUMA… ANGURUMA… NGURUMA..!
Nao mashabiki wa Yanga wamekuwa wakiandika yafuatayo, “Eeh mwenyez mungu tuongoze wanao ktk kaz ya miguu yetu tuanze”.
paschalmusomi “Kesho yanga tupeni raha. Tunakiu ya siku nyingi sana”
Hajimbwambo “Simba hawachezi mpira ila wanaroga tu ila safari hii uchawi wao utadunda”
Chujikabila “yani mnyama anakufa mbili bila”
CAF Champions League
Mamelodi Sundowns and Asfar advance to Quarter-finals
CAF Champions League
TP Mazembe bow out with big win over leaders Al Hilal
CAF Champions League
MC Alger book Quarter-finals spot after draw with Yanga
CAF Champions League
Orlando Pirates capped their incredible with Al Ahly win
Women's Football
FAZ appoints Hauptle as new Copper Queens Coach
Africa Cup of Nations
CAF Slaps Libya with $50,000 fine, Benin also sanctioned
CAF Champions League
Raja Casablanca upset Mamelodi Sundowns
CAF Champions League
Mouth Watering CAF Champions League matches lined up
CAF Champions League
Al Ahly, Al Hilal Omdurman and Esperance looking to book Quarter-finals slot
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...