Connect with us

Matokeo ya michuano ya ligi kuu Afrika Mashariki na Kati

Matokeo ya michuano ya ligi kuu Afrika Mashariki na Kati

 

Michuano ya ligi kuu ya soka Afrika Mashariki iliendelea mwishoni mwa juma lililopita huku vlabu kutoka nchi mbalimbali zikiandikisha matokeo tofauti.

Nchini Kenya, ligi kuu ya Sportspesa iliingia wiki yake ya 9 huku mchuano mkubwa uliovutia mashabiki wengi ukiwa ni kati ya mabingwa watetezi Gor Mahia na Tusker FC.

Tusker 1-0 Gor Mahia (Uwanja wa Nyayo )

Tusker FC ilipata penalti katika dakika ya 77 kipindi cha pili na kuwaangusha mabingwa hao watetezi katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.

Hata hivyo, kulizuka mvutano na mchuano huo kusimamishwa kwa dakika kadhaa baada ya mashabiki wa Gor Mahia kumvamia na kuanza kumpiga refarii msaidizi baada ya kuashiria adhabu hiyo ya penalti.

Bao hilo la kipekee lilitiwa kimyani na kiungo wa Kati wa Tusker Humfrey Mieno.

Tusker wanaotafuta ubingwa msimu huu ni wa pili katika msururu wa ligi kwa alama 20.

278575_heroa

Ulinzi Stars 0-2 Mathare United (Afraha )

Mathare United wakiwa ugenini mjini Nakuru walifanikiwa kupata ushindi muhimu dhidi ya Ulinzi Stars wa mabao 2 kwa 0.

Mathare United kwa sasa wanaongoza ligi kwa alama 20 baada ya mechi 9 na ni ushindi wao wa tatu bila kufungwa bao lolote.

Sony Sugar 1-0 Chemelil Sugar (Awendo)

Hili lilikuwa pambano na wanasukari Magharibi mwa Kenya na Justin Monda aliipa timu yake ushindi wa kwanza msimu huu.

Bandari 1-1 Posta Rangers (Mbaraki Sports Club)

Bandari FC yenye makao yake mjini Mombasa, ikicheza katika uwanja wa Mbaraki ilitoka sare ya bao 1 kwa 1 na wageni wao Posta Rangers kutoka Mombasa.

Bandari FC ilipata bao lake kupitia mchezaji wa zamani wa Mathare United na Gor Mahia Edwin Lavatsa huku Joseph Nyaga akiifungia klabu yake Posta Rangers.

Nchini Tanzania, hali ilikuwa hivyo:-

1763742_heroa

Simba SC 0 Toto Africans 1

Huu ulikuwa mchuano muhimu sana kwa Simba ambayo inataka kunyakua ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu huu baada ya kufanya hivyo mara ya mwisho mwaka 2012.

Kushindwa kwa wekundu wa Msimbazi kumewahuzunisha mashabiki wake na sasa timu hiyo ina alama 57 nyuma ya Yanga FC ambayo inaongoza kwa alama 59.

Hadi sasa Simba wamecheza mechi 25 mchuano mmoja zaidi dhidi ya Yanga.

Yanga 1 Mtibwa Sugar 0

Wanajangwani walirejea kileleni mwa ligi baada ya kupata ushindi muhimu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Yanga wanaongoza kwa alama 59 baada ya kucheza mechi 24.

Coastal Union 1 JKT Ruvu 0

Coastal Union wakicheza wakiwa nyumbani katika uwanja wa Mkwakani mjini Tanga, waliwaangusha maafande wa JKT Ruvu kwa bao 1 kwa 0.

Inashikilia nafasi ya mwisho katika msururu wa ligi kuu ikiwa na alama 22 baada ya mechi 27.

JKT Ruvu ni ya 13 kwa alama 24.

Ndanda FC 2 Kagera Sugar 0

Ndanda FC nayo ilipata alama tatu muhimu baada ya kuwaangusha wanasukari Kagera Sugar mabao 2 kwa 0.

Ndanda FC inashikilia nafasi ya 8 kwa alama 33 huku Kagera Sugar ikiwa ya 12 kwa alama 25.

Coastal Union, African Sports na Mgambo JKT wako hatarini kushushwa daraja msimu huu.

Ligi kuu nchini Uganda

Nchini Uganda, KCCA inaongoza ligi kwa alama 29 baada ya mechi 15.

Vipers inafuata kwa karibu kwa alama 28 huku Police ikiwa ya tatu ikiwa na alama 26.

Uganda

Matokeo kamili ya mwishoni mwa juma llilopita:-

  • Express FC 2 Lweza 0
  • JMC Hippos 0 KCCA 2
  • Sadolin Paints 1 Maroons 0
  • Soana 2 URA 1

Ratiba ya Jumatatu Aprili 18 2016

  • BUL vs URA SC
  • Bright Stars vs Sadolin Paints
  • KCCA vs Saints FC
  • Lweza FC vs Soana

Matokeo ya Super Ligue- Mzunguko wa mwisho nchini DRC

  • Motena Pembe 2 vs Shark XI 1

Ligue A – Burundi

  • Jeunes Athletiques 0 vs LLB Sports 4 Africa 1
  • Inter Star 1 Atletico Olympic 0
  • Ligi kuu nchini Rwanda
  • Musanza 0 Sunrise 1
  • Police Mukura 1 Victory Sports 0
  • Rayon Sport 3 Marines 0
  • Rwamagana City 0 AS Kigali 0.
Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in