Connect with us

Yanga imeanza vibaya kampeni ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kufungwa mabao 4-0 na USM Alger.Yanga ilifungwa mabao mawili kila kipindi na Oussama Darfalou, Farouk Chafai, Abderrahmane Meziane na Mohammed Lamine aliyefunga kwa penati dakika ya 90.

Mchezo huo ulichezeshwa na Mwamuzi Daniel Laryea kutoka Ghana.

Mchezo huo wa Kundi D ulichezwa jana katika Mji wa Algers nchini Algeria unaiacha Yanga ikiwa nafasi ya mwisho katika kundi D la michuano hiyo. Rayon Sports na Gor Mahia zina alama moja baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika mchezo uliochezwa Jijini Kigali.

Hali ikoje

USM Alger inaongoza kwa kuwa na alama tatu ikifuatiwa na Gor Mahia na Rayon Sports zenye alama moja moja na Yanga inaburuza mkia kwa kutokuwa na alama yoyote.

Yanga ijiamini, ina nafasi

Licha ya kuwakosa wachezaji wake muhimu katika mchezo huo, Yanga bado ina nafasi ya kurekebisha makosa na kufanya vyema katika mechi zinazofuata hasa mchezo dhidi ya Rayon Sports ambao kwa mujibu wa ratiba utachezwa Mei 16 Jijini Dar es salaam.

Ni muhimu kutumia vyema uwanja wa nyumbani kupata alama tatu na ikiwa yanga itafanikiwa kupata alama tisa katika uwanja wa nyumbani bado itakuwa na nafasi ya kusonga mbele. Haya yote yatategemea maandalizi mazuri, ufanisi na kujituma kwa wachezaji.

USM Alger tishio.

Ni dhahiri kwa matokeo ya jana USM Alger ndio timu tishio kwenye kundi D. Mara nyingi timu za ukanda wa Afrika Mashariki hupata wakati mgumu pindi zinapocheza na timu kutoka kaskazini. Ni dhdhiri waarabu wqana nafasi kubwa kupenya hatua ya robo fainali.

 

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in