Connect with us

Na Fadhili Omary Sizya,

Mbwana Samatta ameisaidia timu yake KRC Genk kufuzu hatua ya makundi Europa League baada ya ushindi wa jumla 9-4 dhidi ya Broendby ya Denmark.

Usiku wa leo alifunga mara moja katika ushindi wa 4-2 ambao Genk iliupata.

Ikumbukwe mechi ya mkondo wa kwanza Broendby walitandikwa 5-2 Samatta akifunga mabao matatu peke ake.

Hatua ya kupangwa ratiba ya makundi itafanyika leo hii jijini Monaco nchini Ufaransa, hati hati ikiwa katika klabu ya Genk kusubiri ratiba huenda wakakutana uso kwa uso na wababe wa England Arsenal na Chelsea.

More in