Connect with us

Na Frederick Nwaka,

Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara itaendelea kesho kwa michezo mitano kuchezwa kwenye viwanja mbalimbali.

Mabingwa watetezi wa taji, Yanga wamesafiri hadi Singida kuchuana na Singida United na ikiwa watashinda watakaa kileleni mwa msimamo.

Kagera Sugar itaikaribisha Tanzania Prisons, Njombe Mji itaipokea Mbao FC ya Mwanza, wakati Azam itapambana na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Ndanda FC iliyopoteza mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar itaipokea Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara.

Jumapili kutakuwa na michezo miwili ambapo Lipuli itachuana na Mwadui ya Shinyanga na Simba SC itakaribishwa na Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

More in East Africa