Timu ya taifa ya Argentina imesitisha mchuano wake wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Israel, uliokuwa umepangwa kuchezwa siku ya Jumamosi.
Mechi hiyo ingechezwa katika uwanja wa Teddy mjini Jerusalem, kabla ya kikosi hicho cha kocha Jorge Sampaoli kwenda Urusi.
Ubalozi wa Israeli nchini Argentina, umethibitisha kusitishwa kwa mchuano huo kwa sababu za kiusalama, hasa baada ya kuwepo kwa wasiwasi wa kulengwa kwa mshambuliaji na nahodha Lionel Messi.
Argentina, imepangwa katika kundi la D pamoja na Iceland, Croatia na Nigeria.
Argentina, itafungua kampeni yake dhidi ya Iceland tarehe 16.
Hata hivyo, leo usiku kuna michuano kadhaa ya Kimataifa ya kirafiki kuelekea katika fainali hiyo.
Nigeria vs Jamhuri ya Czech
Belarus vs Hungary
Norway vs Panama
Ubelgiji vs Misri
Mechi ya ufunguzi wa kombe la dunia itakuwa siku ya Alhamisi tarehe 14 mwezu huu kati ya wenyeji Urusi na Saudi Arabia.