Klabu 16 za bara Afrika, zinashuka dimbani siku ya Jumanne, kucheza mechi za mwisho, hatua ya makundi, kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika.
Kundi A, tayari Al-Ahly ya Misri na Esperance de Tunis ya Tunisia, tayari zimefuzu na mechi zao na matokeo itakayopata haitakuwa na atahri zozote.
Al-Ahly itakuwa nyumbani kucheza na KCCA ya Uganda huku Esperance de Tunis ikimenyana na Township Rollers ya Bostwana.
Kibarua kigumu kipo katika kundi B, kati ya Difaa El Jadidi, ES Setif na MC Alger zote za Algeria. Timu hizi tatu zina alama tano, huku mabingwa wa zamani TP Mazembe wakiwa wamefuzu.
Diffa El Jadidi wanaowakilisha Morocco, itabidi wapate ushindi dhidi ya Mazembe ili kuwa na matumaini ya kusonga mbele.
Mabingwa watetezi Wydad Casablanca tayari wameshafuzu lakini kazi inasalia kwa Horoya ya Guinea, ikiwa na matumaini ya kuishinda Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ili kusonga mbele.
Hata hivyo, Mamelodi Sundowns inaweza kusonga mbele iwapo itashinda mechi ya leo kwa idadi kubwa ya mabao.
Kundi D, Etoile du Sahel ya Tunisia tayari imeshafuzu na kazi inasalia kwa Primero de Agosto ya Angola ambayo ina alama 6 na inahitaji kuishinda Mbabane Swallows ili kufikisha alama tisa.
ZESCO United ya Zambia ambayo ina alama tano, nayo ina fasi iwapo itaishinda Etoile du Sahel katika uwanja wa Levy Mwanawasa mjini Ndola.
Michuano ya mwisho, hatua ya makundi itachezwa siku ya Jumatano, kutafuta klabu nane zitakazomenyana katika hatua ya robo fainali.
Kundi A
Klabu ya Vita Club kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, inahitaji alama moja muhimu itakapocheza na mabingwa wa zamani ASEC Mimosas kuongoza kundi hili, lakini pia kufuzu katika hatua ya robo fainali.
Hata hivyo, kupata alama hii muhimu, itawalazimu mabeki wa klabu hii, kuwa makini na mshambuliaji wa AS Vita Club, ean-Marc Makusu Mundele, ambaye amefunga mabao saba katika mashindano haya msimu huu.
Raja Casablanca ya Morocco inatarajiwa kushinda nyumbani dhidi ya Aduana Stars ya Ghana na kuungana na Vita Club, katika hatua ya robo fainali.
Kundi B
Klabu ya Berkane na Al Masry za Misri zinaongoza kundi hili na zina nafasi kubwa ya kufuzu katika hatua ya robo fainali.
Berkane kutoka Morocco itaikaribisha UD Songo ya Msumbiji, huku Al Masry ikiwa wenyeji wa Al Hilal ya Sudan.
UD Songo na Al Hilal, ambayo imekuwa ikishiriki katika mashindano haya kwa muda mrefu, haijapata ushindi wowote katika mechi tano zilizopita.
Kundi C
CARA Brazzaville ya Congo, inaongoza kundi hili kwa alama tisa sawa na Enyimba ya Nigeria.
Williamsville ya Ivory Coast nayo bado ina nafasi ya kufuzu iwapo itapata ushindi dhidi ya Djoliba ya Mali na kuungan ana Enyimba, iwapo wawakilishi hawa wa Nigeria watapata ushindi au hata kwendsa sare.
CARA inacheza na Enyimba, ikiwa na historia mbaya ya kushindwa zake zoye za ugenini na hivyo kutoa matumaini kwa Williamsville.
Kundi D
Mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini Kenya Gor Mahia nayo itakuwa ugenini kumenyana na USM Alger, ya Algeria.
Timu zoye mbili zina alama nane, baada ya mechi tano.
Kutokana na rekodi mbaya ya Gor Mahia ugenini, kuna uwezekano ikafungwa na USM Alger na kutoa nafasi kwa APR ya Rwanda ambayo itamenyana na Young Afrucans ya Tanzania jijini Kigali.
Gor Mahia inahitaji kupata alama tatu muhimu ugenini, kujihakikishia nafasi ya kufuzu katika hatua ya robo fainali, la sivyo Rayon Sport washindwe kupata ushindi nyumbani dhidi ya Young Africans.