Connect with us

 

Klabu ya soka ya Medeama FC ya Ghana, imejiongezea matumaini ya kufuzu katika hatua ya nusu fainali kuwania taji la Shirikisho barani Afrika, baada ya kuishinda TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Ikicheza nyumbani katika uwanja wa Sekondi-Takoradi Magharibi mwa nchi hiyo, Medeama waliifunga Mazembe mabao 3 kwa 2, na kujipatia alama tatu muhimu.

Matokeo haya yamefifisha kabisa matumaini ya Yanga FC ya Tanzania ambayo iliishinda MO Bejaia ya Algeria kwa bao 1 kwa 0 na kuanza kupiga mahesabu ya uwezekano wa kusonga mbele.

Licha ya kufungwa ugenini, TP Mazembe inaendelea kuongoza kundi la A kwa alama 10, ikifuatwa na Medeama ambayo ina alama 8.

MO Bejaia ina alama 5, huku Yanga ambayo imeshaondolewa ikiwa ya mwisho kwa alama nne.

Mechi za mwisho za kundi hili zitachezwa mwishoni mwa wiki ijayo.

TP Mazembe itakuwa nyumbani kumenyana na Yanga FC ya Tanzania, huku MO Bejaia ikiikaribisha Medeama FC.

Vlabu vitakavyomaliza katika nafasi ya kwanza na ya pili, vitafuzu katika hatua ya nusu fainali.

Matokeo ya kundi B, mwishoni mwa wiki iliyopita:-

Al-Ahli Tripoli (Libya) – FUS Rabat (Morocco) 1.

Etoile du Sahel (Tunisia) 3 – Kawkab Marrakech (Morocco) 1.

FUS Rabat na Etoile du Sahel, zimejiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu katika hatua ya nusu fainali.

FUS Rabat inaongoza kundi hili kwa alama 11, huku Etoile du Sahel ikiwa ya pili kwa alama 10.

Katika taji la klabu bingwa, Wydad Casablanca kutoka Morocco, ZESCO United ya Zambia na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini zimejikatia tiketi kucheza katika nusu fainali.

Matokeo ya mwishoni mwa wiki iliyopita:-

Al-Ahly (Misri) 2 – ZESCO United (Zambia) 2

Wydad Casablanca (Morocco) 2-ASEC Mimosas (Ivory Coast) 1

Ratiba ya michuano ya mwisho wiki ijayo:-

ASEC Mimosas vs Al-Ahly

ZESCO United vs Wydad Casablanca

Enyimba vs Mamelodi Sundowns

More in