Fainali za 32 za mataifa ya Afrika zinaanza leo nchini Misri kwa kushirikisha mataifa 24, ikiwa ni mara ya kwanza kihistoria.
Mataifa hayo yamegawanywa katika makundi sita yenye timu nne nne ambapo baada ya kutamatika kwa hatua ya makundi timu 16 zitafuzu kucheza hatua ya 16 bora.
Mchezo wa ufunguzi leo ni baina ya wenyeji Misri dhidi ya Zimbabwe ambao utaanza saa tano usiku majira ya Afrika mashariki sawa na saa nne kwa saa ya Afrika ya kati.
Wageni mbalimbali mashuhuri wameshawasili nchini Misri kushuhudia sherehe na mchezo wa ufunguzi akiwemo rais wa Shirikisho la kandanda duniani FIFA, Gian Infantino, Katibu Mkuu wake Fatuma Samoura.
Aidha viongozi mbalimbali wa kisiasa akiwemo rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi na waziri mkuu mstaafu wa Kenya Raila Amollo Odinga watahudhuria tukio hilo.
Baadhi Dondoo muhimu
Ni fainali za 32 za Afrika tangu kuasisiwa kwa mashindano hayo mwaka 1957
Kwa mara ya kwanza mataifa 24 yatashiriki fainali hizo
Nchi za Burundim Mauritania na Madagascar zimefuzu kucheza fainali hizo kwa mara ya kwanza katika historia
Tanzania inashiriki fainali hizo tangu ilipofanya hivyo mwaka 1980, fainali zilizofanyika nchini Nigeria.
Uganda ni taifa pekee la Afrika amshariki lililowahi kufika hatua ya fainali ya mashindano hayo, mwaka 1978 dhidi ya Uganda.
Misri imeshinda taji la Afrika mara saba na inanuia kushinda mara ya nane katika ardhi ya nyumbani.